CUF wauponda UKAWA, huku wenyewe wakijitoa - Kwanza TV | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

CUF wauponda UKAWA, huku wenyewe wakijitoa

Katibu Mkuu mpya wa Chama Cha Wananchi CUF, Khalifa Suleiman Khalifa, amesema wao kama chama cha Wananchi wameshajitoa kwenye mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi ‘UKAWA’ kwa madai upo hoi na hauna msaada kwao.


Khalifa amesema kwamba, msimamo wa CUF ni kutoshirikiana na UKAWA kwa sababu wabunge wa CHADEMA na wafuasi wake wameshindwa kuwa na ushirikiano katika matatizo waliyokuwa nayo.


Kadhalika ameongeza kwamba huo Umoja wa Katiba ya Wananchi kwa upande wao wanaona kama haupo, hivyo wao wameshajitoa huko.


Ameongeza kwamba kwa muda mrefu Wabunge wa CHADEMA, wamekuwa wasemaji wa wabunge waliokuwa wakimuunga mkono  aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Maalim Seif Sharif, ambaye kwa sasa amehamia chama cha ACT Wazalendo.


“Wabunge wa CHADEMA walikuwa wazungumzaji wa wabunge wa CUF ya Maalim Seif. Sisi tunakwenda mahakamani watu wa CHADEMA wanakuja kutufanyia fujo, ilikuwa ina wahusu nini wakati yale yalikuwa matatizo ya ndani ya chama. Sisi tumeshasema hatuwezi kufanya kazi na UKA... Continue reading ->


Source: Kwanza TVRead More