DANNY LYANGA AFUNGA AZAM FC YATOA SARE 1-1 NA EXPRESS UGANDA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DANNY LYANGA AFUNGA AZAM FC YATOA SARE 1-1 NA EXPRESS UGANDA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
KLABU Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati, Azam FC, leo imeendelea na mechi za kujiweka sawa na msimu ujao ikiwa kambini nchini Uganda, safari hii ikitoka sare ya bao 1-1 na Express.
Mchezo huo uliokuwa mkali na wa aina yake, ulifanyika Uwanja wa Mutesa II, ikiwa ni mechi ya tatu ya kirafiki kwa mabingwa hao kambini nchini humo.
Mechi mbili za awali, Azam FC ilitoka suluhu na URA kabla ya kupoteza kwa kufungwa mabao 4-2 dhidi ya washindi wa pili wa Ligi Kuu Uganda, KCCA.
Azam FC ndio iliyoanza kuliona lango la wapinzani wake kwa bao safi lililofungwa na Danny Lyanga dakika ya 15 akiinyanyua mpira ‘chop’ uliomshinda kipa wa Express, Mutombora Fabian, akimalizia pasi safi ya juu ya kiungo, Mudathir Yahya.

Dakika ya 32 Azam FC ilitengeneza nafasi nyingine nzuri, baada ya Lyanga na Tafadzwa Kutinyu kugongeana vema lakini pasi ya mwisho ya Mzimbabwe huyo inakosa mmaliziaji na mpira kuokolewa na mabeki wa Express.
Azam FC ililazimika kufanya mabadiliko dakika nn... Continue reading ->Source: Bin ZuberyRead More