DANTE NA KOTEI WAPELEKWA KAMATI YA NIDHAMU KWA KUWAPIGA GARDIEL NA TSHABALALA - Bin Zubery | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DANTE NA KOTEI WAPELEKWA KAMATI YA NIDHAMU KWA KUWAPIGA GARDIEL NA TSHABALALA

Na Mwandishi Wetu, DAR ES SALAAM
WACHEZAJI Andrew Vincent ‘Dante’ na James Kotei wote watafikishwa Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa makosa yanayofana, kuwapiga wachezaji wenzao katika mchezo wa Ligi Kuu baina ya mahasimu wa jadi, SImba na Yanga Septemba 30.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), Boniface Wambura Mgoyo amesema kwamba maamuzi hayo yamefikiwa katika kikao cha Bodi Oktoba 5, mwaka huu kupitia taarifa na matukio katika mechi za Ligi Kuu, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) zinazoendelea hivi sasa na taarifa mbalimbali. 

Andrew Vincent 'Dante' atapelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kosa la kumpiga kichwa Mohammed Hussein 'Tshabalala'

Wambura amesema kwamba katika mechi hiyo namba 72 iliyofanyika Uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya 0-0, kiungo Mghana James Kotei wa Simba anapelekwa Kamati ya Nidhamu ya TFF kwa kumpiga ngumi Gadiel Gabriel wa Yanga katika dakika ya 33, tukio ambalo Mwamuzi hakuliona.
Naye beki wa kimat... Continue reading ->


Source: Bin ZuberyRead More