Davido atangaza balaa lingine Ijumaa hii, awanyima uhondo mashabiki wake waliochini ya miaka 18 - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Davido atangaza balaa lingine Ijumaa hii, awanyima uhondo mashabiki wake waliochini ya miaka 18

Kama wewe ni shabiki wa Davido na unavutiwa zaidi na ngoma zake basi habari hii bila shaka itakufanya uione wiki hii ndefu sana kwani ametangaza kuachia single yake mpya ya ‘Nwa Baby’ .Davido kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ametangaza kuachia video hiyo Ijumaa ya Tar 17 Agosti 2018 ambapo amesema kuwa wimbo huo utakuwa kwenye mahadhi ya kiafrika huku akiwaahidi mashabiki wake kutowaangusha.


Kwa upande mwingine video ya wimbo huo naonekana kabisa kuwa itakuwa na shots nyingi za kikubwa kwani tayari imepigwa chapa ya Parental Advisory ambapo wazazi hawataruhusiwa kutazama video hiyo wakiwa na watoto wao.


Hii itakuwa ni single ya pili ya Davido kwa mwaka huu baada ya kufanya vizuri na single yake ya Assurance. Je, unadhani Davido kwa mwaka huu atafanya vizuri kama alivyokimbiza mwaka jana na FIA na Fall?.


The post Davido atangaza balaa lingine Ijumaa hii, awanyima uhondo mashabiki wake waliochini ya miaka 18 appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More