DAWASA WAANZA KUDHIBITI UVUJAJI WA MAJI TABATA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DAWASA WAANZA KUDHIBITI UVUJAJI WA MAJI TABATA

* Yazindua siku tatu za kumaliza tatizo la uvujaji maji katika kata 11.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii. 
Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Mkoa wa Dar es Salaam (DAWASA) wamezindua uzibaji wa mivujo ya mabomba inayomwaga maji katika Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani wakianzia katika maeneo ya Tabata zoezi litakalodumu kwa muda wa siku tatu ikiwa ni katika kutekeleza miradi mbalimbali ndani ya siku 100. 
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Uzalishaji na Usambazaji Maji Mhaandisi Aron Joseph alipozindua mkakati huo wa kuhakikisha maeneo yote yanayotiririsha maji kutoka kwenye miundo mbinu ya Dawasa yanafanyiwa kazi kwa asilimia 90 na kisha kukabidhi kwa Meneja wa Dawasa Mkoa wa Tabata. 
Akielezea zoezi hilo lilioanza leo, Aron amesema kuwa watatembelea maeneo yote ya Tabata yenye kata 11 zinazopata huduma za maji na kupambana na mivujo na tayari wataalamu wameshaingia kazini kwa ajili ya kuyafanyia kazi. "Kuna timu zaidi ya watu 70 katika maeneo 20 tofauti ndani ya Tabata ambapo kuna kata 11 y... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More