DAWASA YADAIWA ZAIDI YA BILIONI MOJA NA BODI YA BONDE LA WAMI/RUVU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DAWASA YADAIWA ZAIDI YA BILIONI MOJA NA BODI YA BONDE LA WAMI/RUVU

Na Chalila Kibuda,Globu ya JamiiMAMLAKA ya Majisafi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa) inadaiwa zaidi ya sh. Bilioni Moja na Bodi ya Bonde la Wami/ Ruvu ikiwa ni kusambaza maji bila kulipia bonde kwa ajili ya uendelezaji wa vyanzo vya maji. 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Afisa wa Maji wa Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu Simon Ngonyani amesema kuwa baadhi ya mamlaka za maji katika mikoa wanatumia bonde la Wami/ Ruvu wamekuwa wakilipa vizuri isipokuwa Dawasa. 
Amesema kuwa licha ya Dawasa kuwa na mikakati ya usambazaji wa maji katika jiji la Dar es Salaam hivyo lazima walipe katika bonde kwa ajili ya kuhifadhi vyanzo vya maji hivyo. 
Ngonyani amesema kuwa maji ambayo wananchi wanapata yanatokana na kuwepo vyanzo vya maji ambavyo vinahifadhiwa na mamlaka zilizopo kazi yake ni kusambaza tu. 
Amesema kufikia deni hilo kwa Dawasa ni kutokana na kila wakipelekewa Ankara zao wanazichukua na kuzihifadhi huku wakiendelea kutoa huduma za maji. 
Amesema kuwa wenye visima wote k... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More