DAWASA YAENDELEA NA MIRADI YA KUSAMBAZA MAJI, KUONGEZA MTANDAO WA MABOMBA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DAWASA YAENDELEA NA MIRADI YA KUSAMBAZA MAJI, KUONGEZA MTANDAO WA MABOMBA

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
MAMLAKA ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam(DAWASA) imesema pamoja na mikakati mbalimbali waliyonayo hivi sasa inatekeleza miradi mbalimbali ya usambazaji maji.
Akizungumza jijini Dar es Salaam Meneja Uhusiano wa DAWASA Nelly Msuya amesema usambazaji huo wa maji unaenda sambamba na kuongeza matenki na mtandao wa mabomba.
Amesema usambazaji huo pia utafanyika zaidi maeneo ambayo hayakuwa na huduma bora na maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya viwanda.Msuya ameongeza mikakati ya DAWASA katika kuendelea kuongeza ufanisi wa usafirishaji, mitambo ya majitaka kwani ina faida mbalimbali.
"Moja ya faida ni kupata maji safi yanayoweza kutumika viwandani kwa kupoozea mitambo au shughuli mbalimbali za umwagiliaji,"amesema Msuya.Akizungumzia baadhi ya changamoto za kimazingira wanazozipata Msuya amesema ni shughuli za kilimo ndani ya hifadhi ya mito ambazo huongeza tope pamoja na kemikali zitokanazo na viwatilifu.
Pia shughuli za ufugaji kwenye vyanzo na makusanyio ya maji na changamoto nyingine ni shughuli za uchimbaji madini ambazo uharibu vyanzo na kuingiza kimekali zenye sumu.Msuya amewahimiza wananchi kutunza vyanzo vya maji huku akiwakikishia DAWASA inaendelea kuboresha huduma ya maji kwenye maeneo ya pembezoni ambayo hayajafikiwa na mtandao rasmi.
Pia kuhakikisha jamii za watu wenye kipato cha chini na kati wanapata huduma kwa gharama nafuu.Kuhusu maadhimisho ya Siku ya Mazingira Duniani ambayo hufanyika kila mwaka ifikapo Juni 5, Msuya amesema wameshiriki kwenye maonesho yaliyofanyika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam hasa kwa kuzingatia maji na mazingira vinakwenda sambamba.
Hivyo amesema ushiriki wao kwenye siku ya mazingira ni muhimu kwani unatoa nafasi ya kuelezea wananchi shughuli ambazo wanazifanya wao kama DAWASA.Kuhusu kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya mazingira duniani kuzungumzia umuhimu wa nishati mbadala,Msuya amesema wanaiunga mkono wa vitendo. Meneja uhusiano wa jamii wa DAWASA,Nel Msuya (kulia) akionesha taaswira ya mradi wa usafirishaji maji katika kilele cha maadhimisho ya wiki ya mazingira Duniani  jijini Dar as Salaam. Baadhi ya wananichi waliotembelea banda la Dawasa wakipata huduma.Meneja uhusiano wa jamii wa DAWASA,Nel Msuya (kulia) akizungumza na Globu ya jamii juu usambazaji wa maji na kuongeza matenki na mtandao wa mabomba na kuendelea kutoa huduma bora katika maeneo yaliyo tengwa kwa ajili ya viwanda,jana jijini Dar as Salaam  katika maadhimisho ya wiki ya mazingira Duniani.


Source: Issa MichuziRead More