DAWASA YAENDESHA MSAKO WA WEZI WA MAJI JIJINI DAR - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DAWASA YAENDESHA MSAKO WA WEZI WA MAJI JIJINI DAR

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (DAWASA) wameendesha zoezi la msako wa kuwakamata wezi wa maji ndani ya mkoa wa Dar es Salaam.
Zoezi hilo linaloendelea kwa kasi limefanikisha kukamatwa kwa mkazi mmoja wa Mbezi Kati aliyetambulika kwa jina la Alhaji Londa ambaye anatuhumiwa kujiunganishia maji na kuyauza kwa wenye magari ya kubeba maji usiku. 
Akishiriki katika zoezi la Kuwasaka wezi hao, Meneja wa Mkoa kazi DAWASA Kawe, Gilbert Massawe ameweza kufanikisha kukamatwa kwa mwizi huyo anayedaiwa kujiunganishia maji zaidi ya mwaka mmoja.Katika kumbukumbu za kiofisi zinaonyesha kuwa Londa alikuwa anadaiwa Tsh. Milioni 1.8 na alisitishiwa huduma tangu mwaka jana hata hivyo alijiunganishia maji kinyemela na kuanza biashara ya kuuza maji usiku. 
Gilbert amemtaka Londa Kujisalimisha kituo cha polisi na kueleza kuwa hatua kali zitachuku dhidi yake.Baada ya DAWASA kufanya uchunguzi na kujiridhisha jana ili vamia nyumbani kwa mtuhumiwa na kukuta kweli... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More