DC ARUMERU AWAFARIJI WANANCHI WA KATA YA MBUGUNI ILIYOKUMBWA NA MAFURIKO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DC ARUMERU AWAFARIJI WANANCHI WA KATA YA MBUGUNI ILIYOKUMBWA NA MAFURIKO

Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mh Jerry Muro amefanya ziara kata ya Mbuguni,iliyokumbwa na changamoto ya mafuriko Aprili Mwaka huu, ambapo amewatembelea wananchi waliokumbwa na mafuriko hayo na kuwafariji kwa kutoka misaada mbalimbali ikiwemo magodoro,mablanketi, vifaa vya kuhifadhia maji dawa za kutibu maji na vyandarua pamoja na vifaa vya chakula kwa kila Kaya 60 zilizoathirika.
DC Muro pia ametoa msaada wa vifaa vya usafi kwa wanafunzi wa Shule ya mbuguni,ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada zinazofanywa na Mh.Rais John pombe Magufuli katika kuhakikisha mtoto wa kike anapata Elimu bora huku akiwa katika mazingira bora ya kusoma.
Wananchi wamemshukuru Mh Rais kwa kumteua Jerry Muro kuwa Mkuu wa Wilaya ambaye tayari ameanza kuwahudumia kwa kuwaletea misaada. 
Pia wananchi wamempongeza Rais Magufuli kwa kuendelea kutafuta wadau mbalimbali wa Maendeleo ambao wameanza kuunga mkono jitihada za serikali hususani katika upande wa kukabiliana na majanga kupitia kazi nzuri inayofanywa na Shir... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More