DC awatangazia kiama wavamizi wa misitu - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DC awatangazia kiama wavamizi wa misitu


Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MKUUwa Wilaya ya Biharamulo Sada Malunde amewataka wote wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika misitu ya hifadhi ya Biharamulo na msitu wa Nyantakara wilayani humo kuondoka mara moja kabla ya kuwachukulia hatua za kisheria.

Malunde ametoa agizo hilo jana Septemba 23 akiwa kwenye msitu wa Nyantakara ambako alienda na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na maofisa wa Wakala wa Misitu (TFS) kwa ajili ya kuona uvamizi na uharibifu mkubwa unaoendelea katika hifadhi za misitu iliyopo wilayani humo.

“Misitu huu unavamiwa kwa kasi kubwa na kuharibiwa na watu wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji kinyume cha sheria, hali hii inatishia zaidi baada ya Serikali kupandisha hadhi mapori tengefu ya Kimisi, Burigi na Biharamulo kuwa Hifadhi za Taifa ambapo kuna sheria kali zinazowabana wananchi kufanya shughuli za kibinadamu.

"Nikiwa kama kiongozi mwenye dhamana ya kusimamia utekelezaji wa sheria. Sitakubali hali hii iendelee, nawataka muondo... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More