DC BAGAMOYO AKUTANA NA WAFUGAJI KATA YA VIGWAZA KWA AJILI YA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DC BAGAMOYO AKUTANA NA WAFUGAJI KATA YA VIGWAZA KWA AJILI YA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI

Mkuu wa Wilaya ya Bgamoyo wa kushoto alipowatembea wafugaji wa kimasai katika mnada wa kuuza mbuzi na ng’ombe katika kijiji cha Chamakweza.
VICTOR  MASANGU, VIGWAZA
KATIKA kukabiliana na wimbi la uvunjifu wa amani katika halmashauri ya Chalinze unaochangiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na migogoro ya ardhi baina na  wakulima na wafugaji hatimaye Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa ameingilia kati sakata hilo kwa kuamua kukutana na jamii ya wafugaji kwa lengo la kuweza kulitafutia ufumbuzi wa kina ili kumaliza kabisa changamoto ya kutokea kwa mapigano.
 Mkuu huyo wa Wilaya akizungumza na wafugaji hao kutoka vijiji mbali mbali vilivyopo katika kata ya Vigwaza  katika mkutano wa hadhara ambao aliuandaa maalumu kwa  lengo la  kuweza kusuluhisha migogoro iliyopo pamoja na kusikiliza kero na  changamoto mbali mbali ambazo zinawakabili  jamii ya wafugaji na ili kuweza kuzitatua.
Aidha  mkuu huyo alisema kwamba amesikitisha sana tukio lililotokea hivi karibu katika kijiji cha Pongwe  ambapo mkulima mmoja  kupoteza maisha baada ya kuchomwa na mkuki kifuani kutokana na ugomvi wa kugombania ardhi, hivyo ameahidi kutoa ushirikiano wa dhati katika pande zote mbili na kuwataka  wananchi kuwafichua watu ambao wanahusika  katika kuchochea migogoro hiyo na ambao  wanahusika katika matukio hayo ya mauaji ili waweze kuchukuliwa hatua kali za kisheria.Wafugaji ambao ni jamii ya kimasai kutoka kata ya vigwaza wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo katika mkutano huo wa hadhara.
Pia katika hatua nyingine alibainisha kwamba lengo la serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha inamaliza tofauti zote baina ya wakulima na wafugaji na kuwataka kuheshimiana na kuepukana na masuala ya mapigano na badala yake watekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria na taratibu zote za nchi ili kuondokana kabisa na migogoro iliyopo.
Naye Makamu Mwenyekiti wa chama cha wafugaji Tanzania Ester Moleta  ameiomba serikali ya awamu ya tano kuhakikisha kwamba inawasaidia kwa ahali na mali kuwapatia elimu juu ya ufugaji bora wa mifugo pamoja na kujifunza sheria na taratibu mbali mbali za matumizi bora ya ardhi kwa lengo la kuweza kuondokana na matatizo ya migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji.
Hama kwa upande mmoja wa wafugaji hao akizungumza kwa niba ya wenzake ambaye pia ni Katibu mkuu mstaafu wa chama cha wafugaji Tanzania (CCWT) George Kifuko amesema kwamba migogoro mingi inayojitokeza inasababishwa na baadhi ya viongozi wa vijiji na vitongoji kuamua kujiuzia maeneo kiholela kinyume kabisa na taratibu na sheria zilizowekwa hivyo ni vema  pindi watakapobainika wakachukulia  hatua kali ili iwe fundisho kwa wengine.
HALMASHAURI ya Chalinze iliyopo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani imekuwa ikikabiliwa  na changamoto kubwa kwa  kipindi cha muda mrefu kutokana na kuibuka kwa  migogoro ya kugombania maeneo ya ardhi baina ya  wakulima na wafugaji ambayo inasababisha kutokea kwa uvunjifu wa amani hivyo jitahada za mkuu wa Wilaya kuzungumza na pande zote mbili kutaweza kusaidia kusuluhisha.


Source: Issa MichuziRead More