DC CHAMWINO AWATAKA MAKOCHA WA TIMU ZA TAIFA KUFIKA VIJIJINI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DC CHAMWINO AWATAKA MAKOCHA WA TIMU ZA TAIFA KUFIKA VIJIJINI


NA Charles James, MICHUZI TV
MKUU wa Wilaya ya Chamwino,Vumilia Nyamoga amesema kuna haja ya walimu wa timu za Taifa kuangalia vipaji ambavyo vinapatikana maeneo ya vijijini.
Hayo ameyatoa wakati akifunga mashindano ya Buchimwe Cup yaliyofanyika katika uwanja wa Shule ya Sekondari Buigiri ambapo mchezo wa fainali ulizikutanisha timu za Buigiri Mission na Songambele.
Mkuu huyo wa Wilaya alisema vijijini kumekuwa na vipaji vya hali ya juu lakini anakosekana mtu wa kuwashika mkono hivyo akawaomba walimu wa timu za Taifa kuifika katika maeneo hayo.
“Waje na hapa kwetu Chamwino kuna vipaji vya hali ya juu naamini hata wale Algeria waliochukua AFCON kupitia vipaji hivi ninavyoviona hapa wasingeweza kutufunga,”amesema.
Kwa upande wake Diwani wa Kata ya Buigiri Mhe Kenneth Yindi ambaye ndie muandaaji wa mashindano hayo amesema ataendelea kuandaa mashindano mbalimbali ya Michezo wilayani humo ili kukuza vipaji vya vijana kwani Michezo imekua ni ajira kubwa iliyobadilisha maisha ya vijana wengi.
" ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More