DC GODFREY CHONGOLO ASEMA KIPAUMBELE CHAKE NAMBA MOJA WILAYANI KINONDONI NI MAPATO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DC GODFREY CHONGOLO ASEMA KIPAUMBELE CHAKE NAMBA MOJA WILAYANI KINONDONI NI MAPATO

Na Said Mwishehe,Globu ya jamiiMKUU  wa Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam Godfrey Chongolo amesema kipaumbele chake namba moja,mbili na tatu ni mapato.
Amesema ili halmashauri  ifanye mambo yake vizuri ni lazima iwe na mapato ambayo yatasaidia katika kufanikisha mambo mbalimbali yakiwamo ya kutatua changamoto zilizopo wilayani Kinondoni.
Chongolo amezengumza hayo leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu ateuliwe na Rais Dk.John Magufuli kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni.
Awali Wilaya hiyo alikuwa Ali Hapi ambaye kwa sasa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Iringa.Chongolo kabla ya kuhamishiwa Kinondoni alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Longido.
"Kwangu mimi kipaumbele changu namba moja ni mapato,kipaumbele changu namba mbili ni mapato na kipaumbele changu namba tatu ni mapato.
" Kwanini? Ni kwasababu ukiwa na mapato unaweza kufanya mambo mengi yakiwamo ya kutatua changamoto zilizopo.
"Kwa mfano kuna malalamiko ya kuwepo kwa makelele mengi kutoka kwenye mabaa lakini ukiwa na fedha itakuwa rahisi wanaohusika na mazingira wakaenda kukagua na kuchukua hatua," amesema Chongolo.
Ametoa maelezo hayo leo wakati anajibu swali aliloulizwa na mtangazaji Baby Kabaye wa Clouds Tv ambaye alitaka kujua mikakati ya Chongolo katika eneo la mapato.
Hivyo amesema unahitaji msuli wa kimapato ili kutatua changamoto,ukiwa na kipato ni rahisi kuwajengea uwezo watumishi kufika kwenye maeneo yenye changoto na kuzitatua kwa wakati.
Amesema inafahamika Wilaya ya Kinondoni huko nyuma ilikuwa inasifika kimapato na anao uhakika mapato yataongezeka kutokana na mikakati ambayo wameiweka.
Amefafanua wao wanaangalia mapato kama sehemu ya kuimarisha utoaji huduma kwa wananchi na kusisitiza miongoni mwa huduma hizo ni pamoja na kuimarisha ulinzi wa wananchi na mali zao.
Akifafanua kuhusu ulinzia anasema amepata nafasi ya kuzungumza na Kamanda wa Polisi Kinondoni na moja ya mipango iliyopo ni kuhakikisha inatengenezwa mifumo ya kuimarisha ulinzi.
Amesema kuwa anatambua changamoto ya uhalifu katika Wilaya hiyo ambapo alielezea huko nyuma namna ambavyo kulikuwa na uhalifu ukiwamo wa wizi wa vifaa vya magari.
"Katika eneo la ulinzi hatutakuwa na msamaha kwa atakayebainika kujihusisha na uhalifu.
"Atachukuliwa hatua na kwa mamlaka niliyonayo mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama.
"Hivyo tumejipanga kuhakikisha kunakuwa na usalama wa kutosha kwa wananchi," amesema Chongolo.
Kwa kukumbusha tu Rais Magufuli katika moja eneo ambalo alipata nafasi ya kuzungumzia ni kuhusu mapato na hiyo ni baada ya Wilaya hiyo kuwa ya mwisho katika mapato.


Source: Issa MichuziRead More