DC Jokate atinga gwanda, aanza na ‘operesheni Jokate’ - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DC Jokate atinga gwanda, aanza na ‘operesheni Jokate’

DC wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo amewataka wote wanaoendesha shughuli za kilimo na ufugaji katika misitu ya Ruvu Kusini na Kazimzumbwi wilayani humo kuondoka mara moja kabla hajatumia nguvu.


Akiwa ndani ya msitu wa Ruvu Kusini Jokate amezindua operesheni ya siku 6 ya kuwaondoa wavamizi na kuipa jila la “Operesheni Jokate”.


Jokate ameyafanya hayo leo Agosti 7 akiwa kwenye msitu wa Ruvu Kusini ambako alienda na Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya na maofisa wa Wakala wa Misitu (TFS) kwa ajili ya kuwaondoa wavamizi waliopo humo.


Amesema lengo lake ni kuwasaka na kuwaondoa wavamizi ambao hawataki kufuata sheria na utaratibu wa hifadhi ya misitu katika msitu wa Ruvu Kusini.T


The post DC Jokate atinga gwanda, aanza na ‘operesheni Jokate’ appeared first on Bongo5.com.... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More