DC JOKATE MWEGELO AWEKA WAZI MADINI YALIYOPO KISARAWE YATAKAVYOWANUFAISHA WANANCHI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DC JOKATE MWEGELO AWEKA WAZI MADINI YALIYOPO KISARAWE YATAKAVYOWANUFAISHA WANANCHI

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Kisarawe mkoani Pwani Jokate Mwegelo ameweka wazi kuwa atapambana kwa juhudi na maarifa kuhakikisha uwepo wa madini katika ardhi ya Kisarawe unaleta tija na neema kwa wananchi wa wilaya hiyo.

Akizungumza kuhusu hilo leo DC Jokate amesema chini ya uongozi wake kuanzia mwishoni mwa mwaka 2018 alianza mchakato wa kufanya Geological Survey/Mapping kwakushirikiana na Geological Survey of Tanzania na Ofisi ya Kamishna wa Madini Ukanda wa Mashariki.

Lengo likiwa kutambua aina ya madini na ubora wake na kiasi ambacho kitapatikana ili kuanza kuweka mikakati endelevu na yenye tija ya muda mrefu kwa wilaya na Taifa kwa ujumla.

Amefafanua madini ambayo wilaya ya Kisarawe imejaaliwa kuwanayo kuwa ni; Madini ya udongo jasi, madini aina ya chokaa, malighafi za ujenzi kama vifusi/mchanga, mawe, na kokoto.

Mwegelo amesema Kisarawe haiwezi kuendelea kuwa masikini na kuwa na upungufu wa huduma muhimu za afya na elimu wakati kuna madini katika ar... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More