DC KAWAWA APIGA MARUFUKU WANAOSHIRIKI KUKARIBISHA MIFUGO KIHOLELA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DC KAWAWA APIGA MARUFUKU WANAOSHIRIKI KUKARIBISHA MIFUGO KIHOLELA


NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO 
MKUU wa wilaya ya Bagamoyo, Zainab Kawawa ametoa onyo kwa baadhi ya viongozi wa vijiji na watendaji wanaoshiriki kukaribisha wafugaji bila utaratibu na waache mara moja ,kwani ndio kichocheo cha uvunjifu wa amani na migogoro baina yao na wakulima.
Aidha, amepiga marufuku wafugaji kuingiza mifugo yao kiholela wilayani humo pamoja na maeneo ya wawekezaji ili kuondoa migogoro inayojitokeza mara kwa mara. 
Rai hiyo aliitoa ,wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na madiwani na watendaji wa halmashauri ya Chalinze na Bagamoyo. 
DC Zainab alieleza  kuwa wapo viongozi wanaokula na wafugaji suala linalosababisha ongezeko la mifugo kwenye maeneo yasiyo rasmi. 
Alisema kuwa, kumekuwa na migogoro kati ya wakulima na wafugaji kutokana na baadhi ya wafugaji kuingiza mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima ama wawekezaji hali inayosababisha mapigano.
“Nasema inatosha, wilaya kwasasa ina mifugo hiyo 300,000 yaani halmashauri ya Chalinze ina ng'ombe 240,000 na Bagamoyo ng'o... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More