DC Kigamboni aipongeza UBA Tanzania, yagawa vitabu - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DC Kigamboni aipongeza UBA Tanzania, yagawa vitabu

MKUU wa Wilaya ya Kigamboni, Sara Msafiri, ameipongeza Benki ya UBA Tanzania kwa mchango mkubwa ambao inatoa kwenye sekta ya elimu kwa kutoa vitabu zaidi ya 15,000 kwa shule za sekondari zote zenye uhitaji wa vitabu zilizopo wilaya humo.
UBA Tanzania kupitia UBA Foundation chini ya mpango wa ‘Read Africa Initiative’, imetoa vitabu hivyo vya fasihi kwenye shule za Serikali zilizopo wilaya mpya ya Kigamboni.
Shule ambazo UBA imetembelea ni Nguva Sekondari, Aboud Jumbe Sekondari na Pemba mnazi Sekondari zote zipo ndani ya wilaya hiyo.
Wengine waliokuwepo kwenye tukio hilo ni Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kigamboni, Ng’wilabuzu Ludigija na Ofisa Elimu wa Wilaya, ambapo uongozi wa benki hiyo uliongozwa na Geofrey Mtawa ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha Biashara ndogondogo na za Kati, Mkuu wa Kitengo cha Dijitali, Asupya Nalingigwa na Ofisa Mawasiliano, Anitha Pallangyo.
“Vitabu hivi vilivyotolewa na Benki ya UBA Tanzania, vitasaidia katika kuwajengea vijana wetu kupenda kujisomea na ku... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More