DC MBONEKO AFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO..AKERWA NA DOSARI HALMASHAURI YA SHINYANGA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DC MBONEKO AFANYA ZIARA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO..AKERWA NA DOSARI HALMASHAURI YA SHINYANGA

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Mhe. Jasinta Mboneko, amefanya ziara ya kukagua ujenzi wa miradi ya maendeleo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga na kukumbana na dosari ambapo baadhi ya  majengo yameanza kutoa nyufa kabla hata ya kuanza kutumika. Mboneko amefanya ziara hiyo leo Juni 18,2019 kwa kukagua ujenzi wa madarasa mawili, matundu ya vyoo pamoja na nyumba mbili za walimu katika shule ya msingi Masunula iliyopo kata ya Usule, Shule ya sekondari Itwangi, kukagua madarasa mawili, shule za msingi Tinde “A” na “B” pamoja kukagua madarasa na matundu ya vyoo kwenye shule hizo  na kukumbana na dosari hizo. Mkuu huyo wa wilaya pia amekagua  huduma za matibabu katika kituo cha afya Tinde. Mradi mwingine alioukagua ni Skimu ya umwagiliaji iliyopo kata ya Nyida ambapo Mboneko ameagiza ukamilishwe kwa wakati kabla ya mvua kuanza kunyesha mwezi Oktoba mwaka huu, ili wakulima wanufaike kwa kulima zao la mpunga na kuwainua kiuchumi. Akikagua miradi hiyo ya ujenzi wa madarasa, nyumba... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More