DC MBONEKO AMWAGA VIFAA VYA SHULE KWA WATOTO WENYE UALBINO BUHANGIJA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DC MBONEKO AMWAGA VIFAA VYA SHULE KWA WATOTO WENYE UALBINO BUHANGIJA


Na Marco Maduhu - Malunde1 blog Shinyanga.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Mhe. Jasinta Mboneko, ametoa msaada wa vifaa vya shule kwenye kituo cha kulea watoto wenye ulemavu ualbino Buhangija Jumuishi kilichopo manispaa ya Shinyanga, kwa ajili ya kuwapatia hamasa ya kusoma kwa bidii ili waweze kutimiza ndoto zao.
Mboneko ametoa msaada huo leo Mei 25, 2019 akiongozana na baadhi ya wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama, pamoja na Ofisa Maendeleo ya Jamii manispaa ya Shinyanga Octavina Kiwone, kwa kutoa msaada huo wa vifaa vya shule kwa watoto hao.
Amesema msaada wa vifaa hivyo vya shule ameshirikiana na marafiki zake wa Kikundi Cha Computer Digital Women cha Jijini Dar es salaam, ambapo wameguswa na watoto hao wenye ualbino, na kuamua kuwasaidia vifaa hivyo,ili kutoa hamasa kwao ya kusoma kwa bidii.
“Vifaa hivi vya Shule nimeshirikiana na marafiki zangu wa kikundi cha Computer Digital Women cha jijini Dar es salaam, ambapo wameguswa na ninyi na kuamua kuwasaidia ili msome kwa bidii na kutimi... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More