DC MJEMA AAGIZA TAKUKURU KUCHUNGUZA FEDHA ZA MRADI URASIMISHAJI ARDHI KIPUNGUNI B - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DC MJEMA AAGIZA TAKUKURU KUCHUNGUZA FEDHA ZA MRADI URASIMISHAJI ARDHI KIPUNGUNI B

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
MKUU wa Wilaya Ilala, Sophia Mjema, ameagiza Taasisi ya Kuzuia ya Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), kuchunguza kamati ya mradi wa ulasimishaji ardhi katika Kata ya Kipunguni B kutokana kuwepo viashiria vya ubadhirifu wa fedha za wananchi katika mradi huo .
Dc Mjema alitoa agizo hilo, Kipunguni wilayani Ilala, jana wakati akipokea kero kutoka kwa wananchi wa eneo hilo, wakidai kuchangishwa fedha kulipia gharama za mradi huo.Wananchi wamedai kuchangishwa Sh. 50,000 kwa utambuzi na Sh. 400,000 na kamati hiyo inayojulika vinondo kwa ajili ya kupimiwa ardhi warasimishiwe makazi yao ikiwemo kupatiwa hati miliki.
Mjema alisema sheria iliyoko ni kwamba wananchi walipishwe Sh.250,000 tu, kwa ajili huduma hiyo kutoka katika kampuni ambazo ziko kisheria."Suala hili naiagiza TAKUKURU ilifanyie kazi kwa kuifanyia uchunguzi kamati hiyo, ikibainika sheri aichukue mkondo wake, lakini utaratibu ni kwamba kampuni yeyote itapima kwa Sh. 250,000 tu si zaidi ya hiyo", alisema Mje... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More