DC MSHAMA ADHAMIRIA KUZIFUTA NGO 's ZA MIFUKONI NA ZINAZOFANYA SHUGHULI KIBABAISHAJI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DC MSHAMA ADHAMIRIA KUZIFUTA NGO 's ZA MIFUKONI NA ZINAZOFANYA SHUGHULI KIBABAISHAJI

NA MWAMVUA MWINYI, KIBAHA 

MKUU wa wilaya ya Kibaha, Mkoa wa Pwani Assumpter Mshama ,amedhamiria kuyafuta mashirika yasiyokuwa ya kiserikali (NGO's) wilayani humo ambayo ni ya mifukoni huku yakifanya shughuli kwa utapeli na ubabaishaji.
Aidha amedai atayaandikia barua ya kujieleza mashirika yale ambayo yaliitwa kwenye kikao chake lakini viongozi wake hawakuweza kutokea ambapo kati ya mashirika zaidi ya 100 yaliyofika yalikuwa 21 pekee.
Assumpter aliseyama hayo wakati wa kikao chake na viongozi wa mashirika hayo ili kubadilishana mawazo na kujua changamoto zinazowakabili katika utendaji kazi wao.
Alieleza, watatoa taarifa kwa wafadhili wao kuwa mashirika hayo ni ya kitapeli na hayafanyi kazi kama wanavyojieleza wanapoomba ufadhili.
"Hawa walioshindwa kuja lazima waandike barua za kujieleza kwa nini hawakufika kwenye kikao na nadhani ndo haya tunayoyasema na wakishindwa kujieleza tutawafuta na tutapeleka taarifa kwa msajili wa mashirika haya ili ayaondoe kwenye usajili," alisisitiza Assumpter.Â... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More