DC NAMTUMBO AZUNGUMZIA ZIARA YA KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU, AMSHUKURU KUCHANGIA UJENZI WA MADARASA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DC NAMTUMBO AZUNGUMZIA ZIARA YA KATIBU MKUU WIZARA YA ELIMU, AMSHUKURU KUCHANGIA UJENZI WA MADARASA

Na Ripota Wetu,Globu ya jamii

MKUU wa Wilaya ya Namtumbo mkoani Ruvuma Sophia Kizigo amezungumzia ziara ambayo imefanywa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi na Ufundi Dk. Leonard Akwilapo ambapo ameshukuru kwa kuchangia ujenzi wa madarasa manne kwa shule za sekondari Wilaya ya Namtumbo.
Ambapo Kizigo amefafanua mchango huo umekuja wakati muhimu hasa kwa kuzingatia kwamba mwaka huu wanatarajia kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza wengi, hivyo kusababisha uhaba wa vyumba vya madarasa.
Akizungumzia ziara ya Katibu Mkuu huyo, leo Januari 12,2018 Kizigo amesema alianza ziara kwa kutembelea semina ya mafunzo iliyohusisha Waalimu wakuu wa shule zote za Msingi 110 zilizopo wilaya ya Namtumbo. 
"Semina hiyo ilihusu mafunzo ya jinsi ya kutumia mfumo mpya wa takwimu unaolenga kusaidia kuwa na takwimu sahihi za shule za msingi nchini," amefafanua.
Aliwahimiza wazingatie mafunzo hayo ili iwe rahisi kwao kuutumia mfumo huo mpya.Pamoja na hayo aliwatia moyo na kuwataka wachape kazi kwani wao nd... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More