DC Ndejembi - Rais Magufuli anatekeleza kwa vitendo aliyoyaahidi 2015 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DC Ndejembi - Rais Magufuli anatekeleza kwa vitendo aliyoyaahidi 2015


Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe Deo Ndejembi (pichani kati) amesema vijana nchini wanapaswa kumuunga mkono Mhe Rais Dk John Magufuli kwa jinsi alivyowaamini kwenye nafasi mbalimbali za uongozi
DC Ndejembi amesema kwa miaka mingi ilikuepo dhana ya vijana kuonekana hawana uwezo wa kuongoza lakini Mhe Rais Magufuli katika Serikali yake ya awamu ya tano ameteua vijana wengi kwenye uongozi kuliko awamu nyingine zote.
Amesema kwa maendeleo ambayo Rais Magufuli ameyaleta ndani ya kipindi kifupi cha miaka minne anapaswa kuungwa mkono na vijana na siyo kulalamika pembeni.
Ndejembi ambaye pia amewahi kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama hicho kupitia Umoja wa Vijana pamoja na Mjumbe wa Baraza Kuu la Wazazi amewataka vijana kumuunga mkono Rais Magufuli na kumsaidia kwenye utendaji wake wa kazi katika kuwatumikia wananchi.
" Mhe Magufuli ndiye Rais wetu na ndiye Mwenyekiti wetu ndani ya Chama, mapinduzi ambayo ameyafanya kwenye Nchi hii yanapaswa kupongezwa kwa kiwango kikubwa sana.
" Leo hii chini ya R... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More