DC PANGANI AAGIZA UCHUNGUZI UFANYIKE MAUAJI YA DEREVA WA BODABODA WILAYANI PANGANI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DC PANGANI AAGIZA UCHUNGUZI UFANYIKE MAUAJI YA DEREVA WA BODABODA WILAYANI PANGANI

MKUU wa wilaya ya Pangani Mkoani Tanga Mhe. Zainabu Abdallah ameagiza vyombo vya ulinzi na usalama wilayani humo kufanya uchunguzi wa kina ufanyike ili kuweza kubainika sababu za mauaji ya dereva wa bodaboda Mohamed Ally alimaarufu kama Sharo aliyekuwa anafanya kazi zake Pangani mjini.  Inadaiwa mauaji ya bodaboda huyo yalitokea jioni ya Septemba 22 mwaka huu na mwili wake kupatikana Jumapili na kuzikwa juzi mara baada ya kukodiwa na watu wasiojulikana ambao walitaka awapeleka Tanga mjini na walipofika njiani wakatekeleza mauaji hayo kwa kumnyonga hadi umauti ulipomkuta na kuchukua pikipiki yake kutokomea kusikojulikana. Akizungumza mara baada ya kuitembelea familia ya marehemu na kutoa pole, Mkuu huyo wa wilaya alisema wamepokea kwa masikitiko makubwa na mshtuko wizi huo na mauaji hayo ya bodaboda ambaye ni kijana mjasiriamali.  “Kijana huyu mkazi wa Pangani ameuwawa kikatili sana kwa kunyongwa na watu wasiokuwa na utu na kuchukua pikipiki aliokuwa akifanyia biashara ….inaumiz... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More