DCB WAJITOSA UDHAMINI NDONDO CUP, YAAHIDI KUTOA ELIMU YA HUDUMA ZA KIBENKI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DCB WAJITOSA UDHAMINI NDONDO CUP, YAAHIDI KUTOA ELIMU YA HUDUMA ZA KIBENKI

Meneja Masoko wa Benki ya DCB Boyd Mwaisame akielezea namba watakavyokuwa wanawafungulia akaunti wachezaji na timu shiriki kupitia zawadi wakatazokuwa wanazitoa.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Uzinduzi wa Michuano ya Ndondo Cup iliweza kufunguliwa rasmi jana kwa timu ya Mabibo Market kuchuana na Keko Furniture uliofanyika kwenye Uwanja wa Kinesi Jijini Dar es salaam.
Katika mchezo huo wa kwanza Mabibo Market waliweza kuondoka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Keko ukiwa ni katika hatua ya makundi ya 32 bora.
Kwenye michuano ya mwaka huu, Benki ya DCB imeweza kudhamini kwa mwaka huu na kuahidi kutoa hela za washindi wa kila mchezo sambamba na mchezaji bora wa mechi.
Akuzungumza baada ya kumalizika kwa mechi hiyo, Meneja Masoko wa DCB Boyd  Mwaisame amesema kuwa kwa mwaka huu wameamua kuja kudhamini michuano hiyo ya Ndondo Cup ikiwa ni pamoja na kutoa hamasa kwa wachezaji na timu kuweza kufungua akaunti za benki ili kuhifadhi fedha zao kwa usalama zaidi.
Boyd amesema kuwa katika zawadi wakat... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More