DED BAGAMOYO APANGA VIKOSI KAZI KUFUATILIA VYANZO VYA MAPATO ILI KUONGEZA MAPATO YA NDANI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DED BAGAMOYO APANGA VIKOSI KAZI KUFUATILIA VYANZO VYA MAPATO ILI KUONGEZA MAPATO YA NDANI

NA MWAMVUA MWINYI, BAGAMOYO
HALMASHAURI ya wilaya ya Bagamoyo, imeanza kusambaza vikosi kazi vya wataalamu ambao watatembelea na kufuatilia vyanzo vya mapato yake ya ndani kujua changamoto zinavyovikabili ili kufikia asilimia 25 ya makusanyo kwa kila robo ya mwaka .
Aidha halmashauri hiyo, imetumia milioni 20 ya mapato yake na nguvu za wananchi ,kujenga makalavati makubwa matatu kata ya Kilomo ,hatua iliyosaidia kupitika kwa barabara na kuongeza mapato ya chanzo cha machimbo ya mchango .
Akielezea walivyojipanga katika eneo la ukusanyaji wa mapato ,mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo ,Fatuma Latu ,alisema ,wamekubaliana kuwe na vikosi kazi kufuatilia japokuwa wapo wakusanya mapato ,kodi kwenye kata .
Alisema, itawezesha kwenda pamoja na mpango mkakati wa kimkoa wa Pwani ,kuwa kila robo ya mwaka kukusanya asilimia 25 na kama usipofikia utoe changamoto halisi iliyosababisha kutofikia lengo hilo .
Latu alieleza ,moja ya majukumu yao ni kuhakikisha halmashauri inakusanya mapato kwa ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More