Dhamana ya SoudyBrown, Maua Sama, Shaffih Dauda pamoja na watuhumiwa wengine kujulikana leo (VIDEO) - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Dhamana ya SoudyBrown, Maua Sama, Shaffih Dauda pamoja na watuhumiwa wengine kujulikana leo (VIDEO)

Muda mchache ujao SoudyBrown, Maua Sama, Shaffih Dauda, MX, MC Luvanda pamoja na watuhumiwa wengine wataletwa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam kwaajili kusikiliza mashitaka yanayowakabili.Ijumaa iliyopita mmoja kati ya mawakili wa wahutumiwa hao, Jebra Kambone akifungua kesi Mahakama ya Kisutu ya kuwaombea wateja wake hao dhamana baada ya kushikiliwa na jeshi la polisi kwa wiki moja. Jaji ambaye nasikiliza shauri hilo namba 13 la mwaka 2018 ni Huruma Shaidi.SoudyBrown na Maua Sama wanashikiliwa na jeshi hilo kwa tuhuma za uidhalilisha nembo ya taifa baada ya kusambaa clips za video zinazowaonyesha watu wakicheza na hela ya Tanzania.
Watuhumiwa wengine wanashikiliwa na jeshi hilo kwa kosa la kutumia mitandao ya kijamii blogs na YouTube bila kuwa na kibali.


The post Dhamana ya SoudyBrown, Maua Sama, Shaffih Dauda pamoja na watuhumiwa wengine kujulikana leo (VIDEO) appeared first on Bongo5... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More