Diamond Platnumz Atangaza Ujio Wa Kolabo Yake na Lil Wayne - Ghafla TZ | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Diamond Platnumz Atangaza Ujio Wa Kolabo Yake na Lil Wayne

Msanii wa Muziki wa Bongo fleva Diamond Platnumz ametangaza ujio wa Kolabo yake na Staa wa rap kutoka Marekani Lil Wayne.


Siku za nyuma kulikuwa na tetesi kuwa Diamond anakuja kufanya Kolabo na wasanii wakubwa duniani baada ya kwenda kukaa Marekani kwa muda wa mwezi mzima.


Siku za nyuma  meneja wake Sallam Sk wakati anafanyiwa mahojiano na kituo cha habri cha Times Fm alifunguka na kusema kuwa kuna kitu kizuri kinakuja baada ya kuulizwa swali juu ya kolabo ya msanii wake ambaye ni Diamond na msanii wa nje na kusema kuwa kuna kolabo inakuja akiwa amefanya na Lil Wayne


Diamond ametangaza habari njema kuwa kolabo inayokuja na msanii mkubwa ni Rapa Lil Wayne ingawa hajatoa maelezo ya zaidi kuhusu Kolabo hiyo Lakini ametoa kionjo kidogo cha ngoma hiyo.


Diamond licha ya kufanya kolabo kadhaa kutoka nje ya nchini mfano Nigeria na nchini nyinginezo kutoka Afrika lakini pia msanii huyo amewahi kufanya ngoma na wasanii kutoka Marekani wakiwemo Neyo nyimbo inayojulikana kama Marry you, Rick Ross... Continue reading ->


Source: Ghafla TZRead More