Diva ataka sakata la unyanyasaji kingono linalomkabili R. Kelly lihamie Bongo, adai mastaa wengi wanafanya ufusika - Bongo5 | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Diva ataka sakata la unyanyasaji kingono linalomkabili R. Kelly lihamie Bongo, adai mastaa wengi wanafanya ufusika

Mtangazaji wa kituo cha Radio cha Clouds FM, Diva The Bawse ameingilia kati sakata la unyanyasaji kingono linalomkabili msanii nguli wa muziki duniani R. Kelly kwa kutaka sakata hilo lihamie Tanzania.

Diva na R. Kelly

Diva The Bawse amesema kuwa mastaa wengi duniani wanafanya maovu ambayo watu wengi hawayaoni, hivyo ni vyema kukaandaliwa vipindi vya runinga ambavyo vitawahoji watu waliowahi kunyanyaswa kingono.

Nimeangalia #survivingrkelly toka juzi sijashangaa sana kiukweli zaidi ya kuumia. Tatizo liko kote. Kwa wazazi hasa. watu wengi ambao ni wanaitwa role model duniani watu maarufu wengi ni wachafu sana. Sana sana sana. Hata hapa Tanzania wapo zikiruhusiwa docuseries kama hizi tutasikia mengi sana na kuna hata watasema mtu anasingiziwa ili achafuliwe sababu pia fans hawa nao bendera fata upepo sana. Kwanza ndio wanapenda mambo ya ajabu .. So mejiuliza all the time ilikuwaje wakawa kimya? Na wasichana nao wakiona watu maarufu shobo nyingi sana zinakuwa … ndio matokeo kam... Continue reading ->


Source: Bongo5Read More