DK. KIKWETE AISHAURI CMSA KUTOA ELIMU KUHUSIANA NA FAIDA ZA HISA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DK. KIKWETE AISHAURI CMSA KUTOA ELIMU KUHUSIANA NA FAIDA ZA HISA

CMSA yairudisha NICOL soko la hisa
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne , Dk.Jakaya Mrisho Kikwete ameishauriwa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA) kutoa elimu kwa watanzania kuhusiana na ununuaji wa hisa katika soko la hisa.
Kikwete ameyasema wakati hafla ya Kampuni ya NICOL kurudishwa katika Soko la Hisa Dar es Salaam(DSE) baada ya kukidhi vigezo vya kisheria kuongia katika soko hilo, amesema CMSA ikitoa elimu kwa wananchi kutafanya kuongeza hamasa ya ununuaji hisa kuliko ilivyo sasa.
Dk.Kikwete amesema kuwa CMSA ikitoa elimu kutafanya kampuni nyingi kuorodheshwa katika soko la hisa na kufanya uwekezaji wa miradi mingine.Aidha amesema kutokana na ukuaji wa teknolojia katika masoko CMSA imeshauriwa kuboresha zaidi manada wa soko la Hisa wakati wa kufungua na kufunga.Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete alisema kwamba lengo la kuisajili Nocol ilikuwa ni kuwasaidia .
"Nakumbuka wakati serikali inauza hisa zake NMB kulikuwa na mjadala mkali wa kuhoji kwanini nicol wapewe asilimia tano, lakini kwa imani kwamba hii ni kampuni ya wazalendo, basi tukachukua uamuzi kuwapa wazalendo," alisema.Kikwete kwamba hakuwahi kuusikia mgogoro wa NICOL wakati wa utawala wake.
"Lengo lilikuwa kusaidia wazawa kujijenga kuichumi na kukuza maendeleo, nimesikia leo (jana) hadithi ya Nicol katika uongozi wangu sikusikia kabisa mgogoro wao," alisema Kikwete.Aidha aliipongeza CMSA kwa utendaji kazi wake, ikiwemo kusimamia kwa madhubuti masoko ya mitaji.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akigonga kengele kwa ajili ya kufungua soko la hisa la Dar es Salaam (DSE) kuingia kampuni ya NICOL.
Kaimu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Masoko na Mitaji ya Dhamana (CMSA), Nicodemus Mkama akitoa maelezo kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kuhusiana na kuingia NICOL katika Soko la Hisa la Dar es Salaam , jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti bodi ya NICOL, Dk. Gideon Kaunda akitoa maelezo kwa Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Dk. Jakaya Mrisho Kikwete kuhusiana na kuingia NICOL katika soko hisa na changamoto walizoweza kukabiliana nazo .
Picha za pamoja za makundi mbalimbali katika hafla ya CMSA kuisajili NICOL kwa mara nyingine
Picha za pamoja za makundi mbalimbali katika hafla ya CMSA kuisajili NICOL kwa mara nyingine.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Source: Issa MichuziRead More