Dk Mengi ataka watanzania kujiamini ujasiriamali - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Dk Mengi ataka watanzania kujiamini ujasiriamali

Na Mwandishi WetuWajasiriamali nchini wametakiwa kujiamini kuwa wanaweza kuletea maendeleo kwa kugundua na kutumia ipasavyo fursa za uwekezaji zilizopo nchini.Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk Reginald Mengi kwenye mazungumzo na wajasiriamali wa Asasi ya Entrepreneur Organization – EO Tawi la Tanzania, waliomwalika awasimulie uzoefu wake katika ujasiriamali na kuhusu Kitabu alichokitunga.Amesema Watanzania hawana budi wajiamini kuwa kwa jitihada zao wanaweza kujikwamua kiuchumi kwa kuwekeza kwenye fursa anuwai  zilizopo nchini, wakati huu ambapo Rais John Magufuli anahamasisha uwekezaji, hususan  wa viwanda, baada ya kuboresha mazingira ya uwekezaji.Alisema hilo linawezekana kwa kujifunza kusema kwamba nitaweza na lazima na kisha kutekeleza uthubutu huo kivitendo.Alisema kwamba yeye akiwa anatoka katika familia maskini aliweza kufanikisha kuwa mfanyabiashara mkubwa kutokana na dhamira yake ya kusema nitaweza na kutekeleza msemo huo kwa vitendo.Aidha alisema aliandika kitabu hicho kama alivyoshauriwa na mtoto wake Rodney ili kuwashawishi watanzania wengi zaidi kuwa na uthubutu na ushauri katika kujikita kwenye ujasiriamali na kutumia fursa.Aidha aliwataka watanzania kujifunza na kuwa wabunifu na watunga sera kuona kama elimu yetu ya sasa inakidhi mahitaji halisi au inatakiwa kuboreshwa ili kusaidia katika harakati za kuipeleka nchi yetu kwenye uchumi wa kati.Alisema hayo wakati akijibu maswali katika mdahalo huo kuhusu elimu na kama elimu yetu inafaa kwa sasa. Alisema kitabu alichotunga kinaelezea uzoefu wake katika ujasiriamali kutokana na ukweli kuwa hata wakati wa kuanzisha IPP ni kuwezesha ubunifu na teknolojia miongoni mwa watanzania. Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi akizungumza na wajasiriamali wa Asasi ya Entrepreneur Organization – EO Tawi la Tanzania, waliomwalika awasimulie uzoefu wake katika ujasiriamali na kuhusu Kitabu alichokitunga ‘I Must, I Can, I Will-The Spirit of Success’ alipokutana nao Hoteli ya Coral Beach, Masaki jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mwenyekiti wa Mafunzo wa Asasi ya EO tawi la Tanzania, Bi. Miranda Naiman. Mmoja wa wajasiriamali hao ambao ni wamiliki wa makampuni  mbalimbali nchini akiuliza swali kwa Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi (hayupo pichani) wakati wa mazungumzo na wajasiriamali wa Asasi ya Entrepreneur Organization – EO Tawi la Tanzania, waliomwalika awasimulie uzoefu wake katika ujasiriamali na kuhusu Kitabu alichokitunga ‘I Must, I Can, I Will-The Spirit of Success’ alipokutana nao Hoteli ya Coral Beach, Masaki jijini Dar es Salaam. Wajasiriamali wa Asasi ya Entrepreneur Organization – EO Tawi la Tanzania, wakimsikiliza Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi (hayupo pichani) alipokuwa akiwasimulia uzoefu wake katika ujasiriamali na kuhusu Kitabu alichokitunga ‘I Must, I Can, I Will-The Spirit of Success’ alipokutana nao Hoteli ya Coral Beach, Masaki jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi akitia saini nakala za kitabu chake ‘I Must, I Can, I Will-The Spirit of Success’ zilizonunuliwa na wajasiriamali hao ambao ni wamiliki wa makampuni  mbalimbali nchini mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika hoteli ya Coral Beach-Masaki, jijini Dar es Salaam. Mwenyekiti Mtendaji wa IPP Dk. Reginald Mengi katika picha ya pamoja na wajasiriamali wa Asasi ya Entrepreneur Organization – EO Tawi la Tanzania huku wakiwa wameshika nakala za kitabu chake ‘I Must, I Can, I Will-The Spirit of Success’ mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika katika hoteli ya Coral Beach-Masaki, jijini Dar es Salaam.


KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Source: Issa MichuziRead More