DKT ABBAS: SERIKALI KUJENGA VITUO VYA AFYA 67 - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DKT ABBAS: SERIKALI KUJENGA VITUO VYA AFYA 67

Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.Serikali imesema ndani ya miaka mitatu inatarajia kujenga vituo vya afya 67 katika maeneo mbalimbali nchini. 
Aidha imesema ndani ya kipindi hicho upatikanaji wa  dawa kwa wastani kuanzia ngazi ya zahanati, vituo vya afya na hospitali nchini umefikia asilimia 90.
Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari Maelezo, Dk. Hassan Abbas, amesema hayo leo Novemba 3.2018 alipokuwa akifungua mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Dar es Salaam (DCPC) yaliyoandaliwa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Akizungumza katika mafunzo hayo, Dk. Abbas amesema serikali imeahidi kuboresha huduma ya afya mijini na vijinini kwani tangu kupata Uhuru imejenga Hospitali 77 na sasa inaenda kujenga vituo 67 na kuhakikisha azma ya kutekeleza Huduma ya afya inatekekezwa.
Akizungumzia upatikanaji wa dawa, Dk. Abbas amesema miaka ya nyuma upatikanaji wa dawa kwa zahanati, vituo vya afya na hospitali il... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More