DKT. ASHATU KIJAJI AAGIZA MFANYAKAZI WA TRA DODOMA ASIMAMISHWE KAZI KWA KUKIUKA MAADILI YA KAZI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DKT. ASHATU KIJAJI AAGIZA MFANYAKAZI WA TRA DODOMA ASIMAMISHWE KAZI KWA KUKIUKA MAADILI YA KAZIBenny Mwaipaja, WFM, Dodoma

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, ameuagiza uongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania-TRA, kumsimamisha kazi maramoja mfanyakazi wake mmoja katika Ofisi ya TRA mkoa wa Dodoma, DANIEL KINGU, kupisha uchunguzi wa kuhusika kwake na tuhuma zinazomkabili za kumbughudhi mfanyabiashara mmoja Jijini humo.

Dkt. Kijaji, ametoa maagizo hayo baada ya kufanya ziara ya kushitukiza kwenye mitaa ya Jiji la Dodoma baada ya kupata malalamiko kutoka kwa mfanyabiashara mmoja kwamba amekuwa akipokea simu za vitisho kutoka kwa mfanyakazi huyo akishirikiana na watu wengine na kumtaka ampelekee shilingi laki 7 za kulipia mashine ya kutolea stakabadhi za kielektroniki (EFD Machine) la sivyo angefungiwa biashara yake.

“Mteja wetu awe salama!! na nitaendelea kufuatilia, lakini kuanzia muda huu Kingu aondoke ofisini, hatuwezi kuwavumilia watu wa jinsi hii hata kidogo kwa sababu kazi ya kuuza EFD machine si yake na anamwambia mteja aend... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More