DKT ASHATU KIJAJI AINYOOSHEA KIDOLE WAKALA WA MAJENGO-TBA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DKT ASHATU KIJAJI AINYOOSHEA KIDOLE WAKALA WA MAJENGO-TBA

Na Benny Mwaipaja, Kasulu, Kigoma

Naibu Waziri wa Fefha na Mipango. Dkt. Ashatu Kijaji, ameiagiza Wakala wa majengo Tanzania-TBA, kutekeleza kwa wakati mradi wa ujenzi wa Ofisi ya Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma ili kuiepusha Serikali kutumia fedha nyingi kutokana na kuongezeka kwa gharama za miradi husika kunakotokana na ucheleweshwaji huo.

Dkt. Kijaji ametoa kauli hiyo baada ya kukagua maendelelo ya ujenzi wa Ofisi mpya za Halmashauri ya Mji wa Kasulu zinazojengwa na Serikali kwa zaidi ya shilingi bilioni 2.5 na kutaarifiwa kuwa TBA, wamechelewa kuanza ujenzi huo kwa zaidi ya miezi 12 wakati fedha zilikwisha tolewa na Serikali.

Aliishauri TBA kujipanga kukamilisha miradi inayopewa na Serikali kwa wakati kwa kuongeza idadi ya wataalam wanaoweza kusimamia miradi mingi inayotekelezwa na wakala huo.

"Pesa zipo, Serikali haiwezi kuanza kutekeleza mradi wowote kama hakuna pesa, ni jukumu lenu kama TBA kuhakikisha mnawezesha mradi huu ukamilike kwa wakati ili tupate ... Continue reading ->
Source: Issa MichuziRead More