DKT. ASHATU KIJAJI: UJENZI WA VITUO VYA AFYA WAPAMBA MOTO NCHINI KOTE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DKT. ASHATU KIJAJI: UJENZI WA VITUO VYA AFYA WAPAMBA MOTO NCHINI KOTE

Benny Mwaipaja, Kasulu, Kigoma 
Serikali imepanga kujenga zaidi ya vituo 120 vya afya nchini kote katika mwaka wa fedha 2018/19 ili kusogeza huduma za afya karibu zaidi na wananchi ikiwemo huduma ya mama na mtoto.

Hayo yamesemwa Mjini Kasulu, mkoani Kigoma na Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, alipotembelea na kukagua ujenzi wa majengo mapya ya Kituo cha Afya Kiganamo, yaliyo gharimu shilingi milioni 500.

Amesema kuwa tangu Serikali ya Awamu ya Tano iingie madarakani imeongeza bajeti ya Wizara ya Afya kutoka shilingi bilioni 30 hadi kufikia shilingi bilioni 369, hatua iliyolenga kuboresha afya za wananchi kwa kuwa hakuna maendeleo kama wananchi watakuwa na maradhi.

“Awamu ya Tano ilianza na ujenzi wa vituo 44 vya afya na kufuatiwa na vituo 74 na sasa vituo takribani 120 vinaendelea kujengwa maeneo mbalimbali ili kutimiza lengo la kuwa na Kituo cha Afya kwa kila Kata”, alieleza Dkt. Kijaji.

Dkt. Kijaji, alisema Serikali imeweka utaratibu wa Kata ambazo zipo jirani kutumia kituo kimoja wakati lengo kuu la kujenga kituo kimoja cha afya kwa kila Kata likiendelea kutekelezwa katika uongozi wa Serikali ya Awamu ya Tano.
Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akifurahia maelezo ya Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma Dkt. Mshana Dastan, kuhusu namna walivyojipanga kuhakikisha kituo hicho kinaanza kutoa huduma kwa wakati kutokana na umuhimu wake kwa wakazi wa Kasulu na maeneo yanayoizunguka Wilaya hiyo. 
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu Mkoani Kigoma, Dkt. Mshana Dastan (kushoto), akitoa maelezo kuhusu ujenzi wa Chumba cha kuhifadhia maiti ikiwa ni sehemu ya majengo mapya yaliyojengwa na Serikali kwa gharama ya shilingi milioni 500, likiwemo jengo la wodi ya akina mama, maabara, nyumba ya mganga na miundombinu mingine, wakati Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb), alipofanya ziara kukagua maendeleo ya ujenzi wa miundombinu ya kituo hicho cha afya. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>


Source: Issa MichuziRead More