DKT BASHIRU: WAZIRI WA VIWANDA ATATUMBULIWA AKISHINDWA KUFUFUA VIWANDA - Mwanaharakati Mzalendo | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DKT BASHIRU: WAZIRI WA VIWANDA ATATUMBULIWA AKISHINDWA KUFUFUA VIWANDA

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Dk Bashiru Ally amesema Waziri wa Viwanda, Innocent Bashungwa atatumbuliwa ikiwa atashindwa kutimiza azma ya Serikali ya kufufua viwanda.


Dk Bashiru ametoa kauli hiyo jana Jumanne Julai 9, 2019 baada ya kutembelea kiwanda cha kukoboa kahawa cha TCCCO kilichopo manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro.
Amesema ajenda ya Serikali ya Awamu ya Tano ni kufufua viwanda na kwamba jambo linalopaswa kufanya ni kujiandaa katika masuala ya ushirika, ubunifu na ujuzi ili nchi iweze kujisimamia.
“Nimesoma katika kitabu cha wageni waziri wa Viwanda alikuwa hapa Mei 28 (aliyekuwa Waziri wa Viwanda, Joseph Kakunda) na ameshatumbuliwa, na huyu aliyepo ajiandae kutumbuliwa maana kama tunasema tunahitaji uchumi wa viwanda halafu havifufuki.”
“Barabara zinajengwa unaziona, SGR (Reli ya kisasa) unaiona, kwa nini hatuoni viwanda vinafufuliwa?” amehoji Dk Bashiru.
Amesema kuendesha kiwanda kama TCCCO ni lazima kuwepo na kiwanda cha magunia, “Bado kun... Continue reading ->Source: Mwanaharakati MzalendoRead More