Dkt. Kalemani aagiza ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Geita uanze mwezi wa Sita - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Dkt. Kalemani aagiza ujenzi wa kituo cha kupoza umeme Geita uanze mwezi wa Sita

Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani akiwasha umeme katika Kijiji cha Mnadani wilayani Sengerema, kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Emmanuel Kipole.
Na Teresia Mhagama, Geita
Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani, amemwagiza mkandarasi wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme wilayani Geita, kuanza ujenzi wa kituo hicho mwezi wa Sita  mwaka huu na kumaliza kazi hiyo mwezi wa Tano mwakani ili kuboresha hali ya umeme mkoani Geita.
Dkt Kalemani aliyasema hayo wakati akiwa kwenye ziara ya kukagua miradi ya umeme inayoendelea kutekelezwa katika Mkoa wa Mwanza na Geita ambapo alikagua kazi ya ujenzi wa kituo cha kupoza umeme wilayani Geita na mradi wa usambazaji umeme vijijini  wilayani Sengerema na Chato.
"Msisubiri kusukumwa, jitumeni wenyewe ili mradi huu ukamilike mapema, na wananchi wapate umeme usiokatika mara kwa mara,  pia kukamilika kwa kituo hiki kutawezesha mgodi wa dhahabu wa Geita kuunganishwa na umeme wa gridi, kwani sasa wanatumia umeme wa mafuta ambao ni wa gharama kub... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More