Dkt Kalemani Aendelea Kuwasha Umeme Vijijini - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Dkt Kalemani Aendelea Kuwasha Umeme Vijijini

Afanya ziara wilayani Handeni, Lushoto na kuwasha umeme katika Vijiji Vitano

Katika kuhakikisha kuwa adhma ya Serikali ya kusambaza umeme katika vijiji vyote nchini ifikapo mwaka 2021 inatekelezwa, Waziri wa Nishati, Dkt Medard Kalemani amefanya ziara katika Wilaya ya Handeni na Lushoto mkoani Tanga ili kukagua kazi za usambazaji umeme vijijini na kuwasha umeme katika baadhi ya vijiji.

Akiwa wilayani Handeni, Waziri wa Nishati aliwasha umeme katika Kijiji cha Madebe, Nyasa na Kwamnele na wilayani Lushoto aliwasha umeme katika Kijiji cha Mabugai na Nkelei. Aidha alifanya ziara katika kata na Vijiji mbalimbali ambavyo bado havijasambaziwa umeme ikiwemo Kijiji cha Mahezangulu kilicho katika Jimbo la Bumbuli, wilayani Lushoto ambapo aliagiza kuwa, kiwashiwe umeme ifikapo tarehe 12 mwezi huu.

Katika ziara yake wilayani Handeni, Viongozi wa Wilaya hiyo walimweleza kuwa, kuna vijiji 10 ambavyo vimepitiwa na miundombinu ya umeme lakini havina nishati hiyo, hivyo kuleta malala... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More