DKT. KIJAJI AAGIZA DEREVA ALIYEHAMISHWA KITUO CHA AFYA BITALE KIGOMA KURUDISHWA MARA MOJA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DKT. KIJAJI AAGIZA DEREVA ALIYEHAMISHWA KITUO CHA AFYA BITALE KIGOMA KURUDISHWA MARA MOJA


Na Benny Mwaipaja, WFM, Kigoma.

NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmahauri ya Wilaya ya Kigoma kumrejesha mara moja katika kituo chake cha kazi cha awali, dereva wa Kituo cha Afya Bitale, kilichoko Kata ya Bitale katika Halmashauri ya wilaya hiyo baada ya kubainika kuwa gari la kubeba wagonjwa kituoni hapo halina dereva.
Dkt. Kijaji, ametoa maelekezo hayo alipotembelea Kituo hicho cha Afya kukagua ujenzi wa majengo mapya ya Kituo hicho yatakayogharimu shilingi 400m  baada ya Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Bitale, Dkt. Norbert Nshemetse, kueleza changamoto ya upungufu wa watumishi wa kituo hicho akiwemo dereva.
Dkt. Nshemetse, pamoja na kumshukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, kwa kuwapatia gari la wagonjwa (Ambulance) katika kituo hicho, alisema gari hilo halina dereva baada ya dereva wake kuhamishiwa katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma mwezi Julai, 2018.
“Katika... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More