DKT. KIJAJI AWATAKA WAFANYABISHARA KIGOMA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIBIASHARA NA NCHI JIRANI ZA BURUNDI NA RWANDA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DKT. KIJAJI AWATAKA WAFANYABISHARA KIGOMA KUCHANGAMKIA FURSA ZA KIBIASHARA NA NCHI JIRANI ZA BURUNDI NA RWANDA

Benny Mwaipaja, Kakonko, Kigoma
NAIBU Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Ashatu Kijaji, amewashauri wakazi wa Wilaya ya Kakongo na mkoa wa Kigoma kwa ujumla kuchangamkia fursa za biashara kati ya mkoa huo na nchi jirani za Rwanda na Burundi kwa kuuza mazao ya kilimo yaliyochakatwa likiwemo zao la muhogo ili waweze kunufaika na biashara hiyo ya mipakani.
Dkt. Kijaji ametoa rai hiyo mjini Kakonko baada ya kukutana na kufanya mazungumzo na wafanyabiashara wa wilaya hiyo, mkutano uliolenga kujadili fursa na changamoto za ufanyaji biashara katika eneo hilo yakiwemo masuala ya kikodi.
"Nakuomba Mkuu wa Wialaya ya Kakonko uwakutanishe na kuwaunganisha wafanyabiashara hawa ambao nafurahi wengi wao ni vijana ili waandae andiko la namna ya kununua mashine za kuongeza thamani ya mazao ili wauze nje yakiwa yamechakatwa badala ya mfumo wa sasa ambao wanauza mazao ghafi nje ya nchi na hivyo kupata hasara" alisisitiza Dkt. Kijaji
Awali, wafanyabiashara wa Kakonko walimweleza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More