DKT. KIKWETE ASIMULIA KILICHOPELEKEA KUANDIKA KITABU CHAKE, KUANZISHA TAASISI YAKE - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DKT. KIKWETE ASIMULIA KILICHOPELEKEA KUANDIKA KITABU CHAKE, KUANZISHA TAASISI YAKE

RAIS Mstaafu wa Awamu ya Nne na Mwanzilishi wa Taasisi ya Jakaya Kikwete Dkt. Jakaya  Kikwete amesema kuwa  taasisi yake pamoja na kitabu chake cha The Journey Of My Life alifikiria kuanzisha vitu ambavyo vitakuwa kumbukizi kabla ya kumaliza uongozi wake akiwa kama Rais.
Dkt. Kikwete ameyasema hayo jijini Dar es Salaam katika hafla maalum ya Chakula cha jioni iliyoandaliwa na Chemba ya Biashara ya Marekani hapa nchini (AMCHAM) kwa lengo yakuishukuru Serikali ya Tanzania.
Amesema katika uongozi wake marafiki  walifikiri jambo ambalo atalifanya mara baada ya kumaliza utumishi wa umma aliohudumu kwa miaka 40, ambapo alitaka kuweka uzoefu na mawazo yake katika maandishi ili yasiweze kufutika.
Kikwete amesema katika kitabu cha The Journey of My Life  ameeleza kuhusiana na taasisi ya Jakaya na maisha yake tangu akiwa mdogo huko kijijini Msoga pamoja na uzoefu wa uongozi kwa miaka 40.
Dkt. Kikwete amesema katika kitabu chake amegusia maeneo mbalimbali yakiwemo kilimo, afya, vijana na utawala... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More