DKT. MABODI AFANYA ZIARA MANISPAA YA MJINI ZANZIBAR - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DKT. MABODI AFANYA ZIARA MANISPAA YA MJINI ZANZIBAR

NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi, amesema CCM imendelea kusimamia kwa ufanisi sera za maendeleo kwa jamii bila kujali itikadi za kisiasa. Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na Watendaji wa Baraza la Manispaa Mjini, huko Sebleni katika mwendelezo wa ziara yakeb ya kukagua miradi mbali mbali iliyotekelezwa na manispaa chini ya mfumo wa Ugatuzi.
Dk.Mabodi ameeleza kwamba mipango endelevu inayotekezwa na Serikali za mitaa kwa lengo la kuimarisha huduma muhimu za kijamii katika nyanja za afya,elimu,uvuvi,ufugaji,kilimo na ujasiriamali ni kwa ajili ya wananchi wa rika zote bila ya kubaguliwa. Ameeleza kuwa Serikali Kuu imeamua kupeleka madaraka katika Serikali za Mitaa kwa lengo kurahisisha upatikanaji wa huduma bora za kijamii kwa wananchi.
Ameeleza kwamba utekelezaji mzuri wa mipango iliyomo katika ugatuzi ndio litakuwa ni chimbuko la utengenezwaji wa Ilani ya uchaguzi ya mwaka 2020/2025, iliyokuwa bora na inayo... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More