Dkt. Mahiga amwakilisha Rais Magufuli katika Mkutano Maalum Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

Dkt. Mahiga amwakilisha Rais Magufuli katika Mkutano Maalum Wakuu wa Nchi na Serikali wa AU

Mhe. Augustine P. Mahiga (Mb), Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki alimwakilisha Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye Mkutano Maalum wa 11 wa Wakuu Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliyofanyika tarehe 17-18 Novemba, 2018 mjini Addis Ababa, Ethiopia. Mkutano huo, uliitishwa kufuatia maamuzi ya Mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika uliofanyika mwezi Julai 2018 mjini Nouakchott, Mauritania ambapo Wakuu hao walielekeza uitishwe Mkutano Maalum kujadili kwa kina mabadiliko ya kitaasisi ndani ya Umoja huo. 
Mkutano huo ulijadili na kutolea maamuzi mapendekezo kuhusu Muundo wa Uongozi (Portfolios) za Kamisheni za Umoja wa Afrika; chaguzi za Uongozi wa Kamisheni; Kusitisha ajira za viongozi wa Kamisheni; na Mabadiliko ya kiutawala na fedha ikijumuisha utendaji.Mkutano ulikubaliana kupunguza idadi ya wajumbe wa Kamisheni klutoka 10 hadi 8 ambao ni Mwenyekiti wa Kamisheni, Makama Mwenyekiti na Makamis... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More