DKT MPANGO: MAREKEBISHO YA SHERIA YA TAKWIMU HAYAZUII KUFANYA TAFITI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DKT MPANGO: MAREKEBISHO YA SHERIA YA TAKWIMU HAYAZUII KUFANYA TAFITI


Na. WFM Mjini Bali Indonesia

Marekebisho ya Sheria ya Takwimu ya Mwaka 2018, hayawazuii wadau wa takwimu kutoa takwimu kwa ajili ya matumizi yao bali marekebisho hayo yanaweka misingi ya kuzingatiwa wakati wa utoaji wa takwimu hizo.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Isdor Mpango, alipofanya mkutano na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Fedha (IMF) anayewakilisha Tanzania na nchi nyingine (Africa Group 1 Constituency), Bw. Maxwell Mkwezalamba, katika Mikutano ya Benki ya Dunia (WB) na Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) mjini Bali Indoneshia.

Dkt. Mpango amesema kuwa lengo la marekebisho ya sheria hiyo ni kurahisisha ufanyaji wa tafiti na utoaji wa matokeo ya tafiti na sio kuwabana wadau katika ukusanyaji wa taarifa za kitakwimu au kuzuia mijadala ya uchambuzi wa kisera wa matokeo ya takwimu rasmi.

“Tumekubaliana kutumia fursa ya kuboresha Kanuni za Takwimu kwa ajili ya kuweka mazingira ya utekelezaji mzuri wa vipengele vya sh... Continue reading ->

Source: Issa MichuziRead More