DKT NDUGULILE AITAKA SEKTA YA AFYA KIGOMA KUTOA ELIMU KUHUSU UGONJWA WA EBOLA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DKT NDUGULILE AITAKA SEKTA YA AFYA KIGOMA KUTOA ELIMU KUHUSU UGONJWA WA EBOLA

Na Editha Karlo,Michuzi TV.
NAIBU Waziri wa afya,maendeleo ya jamii jinsia wazee na watoto Faustin Ndugulile ameitaka sekta ya afya Mkoani Kigoma kutoa elimu kwa watumishi wote wa afya kutambua hatua za kukabiliana na ugonjwa wa Ebola
Ndugulile amesema kuwa endapo elimu itatolewa kwa wakati ikiwa ni sambamba na kushirikiana na vyombo vya ulinzi na usalama na kuwashirikisha wananchi kikamilifu ugonjwa wa Ebola utathibitiwa kwakuwa kila mmoja atakuwa anafahamu namna ya kuutambua ugonjwa huo.
"Elimu ikitolewa kwa wakati kwa kuwashirikisha wananchi kikamilifu ugonjwa wa Ebola tutaweza kuuthibiti kwani kila mtu anakuwa anaufahamu baada ya kupata elimu"alisema 
Pia alisema kuwepo na uangalizi katika mipaka ili kuzuia watu kuingia kutoka nchi za jirani na kuingia nchini kiholela.Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga amesema Mkoa wa Kigoma unachangamoto ya mipaka,lakini hatua mbalimbali zinachukuliwa kuthibiti wanaoingia kihohela nchini.
Naye Mganga Mkuu wa... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More