DKT. NDUGULILE AWAAGIZA KUFUATILIA MTOTO ALIYEKATWA MKONO MWANANYAMALA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DKT. NDUGULILE AWAAGIZA KUFUATILIA MTOTO ALIYEKATWA MKONO MWANANYAMALA

Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza wakati wa uzinduzi wa bodi ya maabara binafsi za afya kwenye ukumbi wa hoteli ya Veta jijini Dodoma.
Na. Catherine Sungura –DodomaNAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee wa Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amemuagiza Msajili wa  Baraza la Madaktari la Tanganyika kushirikiana na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania kufuatilia mtoto aliyekatwa mkono baada ya kuhamishiwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili kutoka hospitali ya rufaa ya mkoa ya Mwananyamala.
Dkt. Ndugulile ametoa maagizo hayo wakati akizindua bodi ya nane ya maabara binafsi za afya kwenye ukumbi wa Veta jijini hapa.
“Nilitegemea baraza la madaktari muwe mmeanza uchunguzi, kwahiyo nakupa maagizo kesi hiyo muanze kufuatilia na kama itathibitika ni uzembe waliohusika wachukuliwe hatua, ndani ya wiki mbili mtuletee majibu ili mimi na Mhe. Waziri tujue tunachukua hatua gani.
Dkt. Ndugulile amesema kwenye mabaraza bado... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More