DKT TIZEBA ATANGAZA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA KUFANYIKA MKOANI SIMIYU KWA MIAKA MITATU MFULULIZO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DKT TIZEBA ATANGAZA MAONESHO YA NANENANE KITAIFA KUFANYIKA MKOANI SIMIYU KWA MIAKA MITATU MFULULIZO

Na Mathias Canal, WK-Simiyu
Waziri wa kilimo Mhe Dkt Charles Tizeba ametangaza kuwa maadhimisho ya maonesho ya kilimo na sherehe za wakulima Nanenane Kitaifa yatafanyika Mkoani Simiyu kwa miaka mitatu mfululizo kuanzia mwaka 2018 mpaka 2020 ili kuongeza tija ya elimu kuhusu sekta ya kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa wananchi wa kanda ya Ziwa Mashariki.
Waziri wa kilimo Mhe Tizeba ametanga neema hiyo kwa wananchi wa kanda ya ziwa Mashariki jana tarehe 8 Agosti 2018 kwa wakazi wa mikoa ya Simiyu, Shinyanga na Mara ambayo inaunda kanda ya ziwa Mashariki ambao watanufaika na elimu kuhusu kilimo, mifugo na uvuvi.
Alisema kuwa kumekuwa na utaratibu wa kufanyika mfululizo maonesho hayo kwenuye mikoa inayoandaa huku akieleza kuwa utashi uliopo katika kanda hiyo ni mkubwa ukilinganisha na maonesho ya Nanenane yaliyofanyika kwa miaka minne mfululizo katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Alisema kuwa kufanyika mfululizo kwa miaka mitatu mkoani Simiyu kutawafanya wananchi kuwa na uhakika wa bidhaa za uwek... Continue reading ->Source: Issa MichuziRead More