DKT TIZEBA AWASILISHA TAARIFA YA ZAO LA KAHAWA KWA KATIBU MKUU CCM, USHIRIKA WAUNGWA MKONO KWA KAULI MOJA - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DKT TIZEBA AWASILISHA TAARIFA YA ZAO LA KAHAWA KWA KATIBU MKUU CCM, USHIRIKA WAUNGWA MKONO KWA KAULI MOJA

Na Mathias Canal-WK, Dodoma
Katika vipindi mbalimbali vya historia ya Tanzania masoko ya Kahawa yamekuwa yakiendeshwa kwa mfumo wa ushirika na soko huria, Mfumo wa soko huria uliruhusu makampuni na watu binafsi kununua mazao moja kwa moja kutoka kwa wakulima pasipo udhibiti hali iliyopelekea kuwepo kwa changamoto mbalimbali zikiwemo bei isiyokuwa na tija kwa mkulima, ubora hafifu wa mazao, ukwepaji wa kodi kwa wanunuzi na ukosefu wa takwimu sahihi za uzalishaji na mauzo.


Kutokana na changamoto za mfumo wa soko huria, Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli iliamua kurejesha ununuzi wa mazao matano ya kimkakati (Korosho, Tumbaku, Pamba, Kahawa, na Chai) kupitia vyama vya ushirika tangu mwaka 2016 ili kunufaisha wakulima, wanunuzi/wafanyabiashara na serikali.


Hayo yamebainishwa jana tarehe 14 Septemba 2018 na Mhandisi Mhe Dkt Charles Tizeba, Waziri wa kilimo wakati akiwasilisha taarifa ya mwenendo wa soko la kahawa nchini ... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More