DKT TIZEBA AWATAKA WAKULIMA WA NYANYA IRINGA KUCHANGAMKIA FURSA YA UZALISHAJI SOKO LIPO - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DKT TIZEBA AWATAKA WAKULIMA WA NYANYA IRINGA KUCHANGAMKIA FURSA YA UZALISHAJI SOKO LIPO

Na Mathias Canal-WK, Mseke-IringaWAZIRI wa Kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb), amewataka wakulima wa nyanya Mkoani Iringa kuchangamkia fursa ya kuongeza uzalishaji wa nyanya ili kuakisi uhitaji wa viwanda vya nyanya ikiwa ni pamoja na kiwanda cha Darsh chenye uwezo wa kusindika Tani 250 za nyanya kwa siku.


Waziri Tizeba ametoa mwito huo jana Octoba 18, 2018 wakati akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda cha Darsh kilichopo Kijijini Igwachanya Kata ya Mseke katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa.


Kiwanda hicho kinafanya shughuli za ukusanyaji wa nyanya kutoka maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Iringa na mikoa ya jirani na kufanya usindikaji wa nyanya ambapo hupeleka kiwanda cha Arusha kwa ajili ya uzalishaji wa bidhaa zinazotokana na nyanya ambazo huuzwa ndani na nje ya nchi.


Waziri Tizeba, aliwataka wakulima hao kujiunga kuanzisha kikundi cha ushirika ili kuwa na urahisi wa mikopo ili kuwezesha uwezo wa uwekezaji kupitia kilimo cha umwagiliaji kitakachoongeza tija katika kipato chao n... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More