DPP AWATAKA WADAU WOTE WASHIRIKI KATIKA MAPAMBANO YA UJANGILI KWA WANYAMAPORI - Issa Michuzi | PressTZ - Your Number 1 Source of Aggregated Online Content

 

DPP AWATAKA WADAU WOTE WASHIRIKI KATIKA MAPAMBANO YA UJANGILI KWA WANYAMAPORI

Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
MKURUGENZI wa Mashitaka nchini (DPP), Biswalo Mganga amesema juhudi mbalimbali za wadau wakiwemo mashahidi pamoja na mawakili wa pande zote mbili  katika kesi ya kujihusisha na mtandao wa uhalifu wa nyara za serikali, Yang Glan maarufu Malkia wa Meno ya tembo  wenzake ndizo zimefanikisha washitakiwa hao kutiwa hatiani . 
Ameyasema hayo leo Februari 19, 2019 wakati akizungumza na wanahabari mara baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo ambapo amesema ni muhimu kwa wadau wote nchini  kuongeza ushirikiano katika mapambano dhidi ya vitendo vya ujangili ambavyo kwa kiasi kikubwa vimelisababishia taifa hasara hasa katika upotevu wa maliasili muhimu hususani wanyamapori kama tembo na wengineo. 
 Amesema Watanzania wanapaswa kuzilinda maliasili zote zilizopo nchini kwani wakishindwa kufanya hivyo ipo hatari ya kupotea na watalii kutokuja tena Tanzania hali itakayosababisha pato la taifa kushuka.
Hata hivyo, amesema kwa upande wa kiuchumi madhara yatokanayo na uja... Continue reading ->


Source: Issa MichuziRead More